Alhamisi , 12th Sep , 2019

Jayesh Patel raia wa India mwenye miaka 32, amekamatwa na polisi kwa kosa la kujifanya babu wa miaka 81 ili kupata nafasi ya kwenda nchini Marekani.

Jayesh Patel

Jamaa huyo alikamatwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege ujulikanao kama 'Gandhi International Airport' siku ya Jumapili baada ya kukaguliwa na ofisa usalama.

Polisi wamesema jamaa huyo alifika Airport wakati wa kukaguliwa akiwa anatembea katika kiti cha magurudumu ya vilema na alipaka ndevu rangi nyeupe, miwani ya kizee na alijifunga vilemba ili aonekane mzee.

Aidha  polisi wameendela kusema Passport yake ilionyesha anaitwa jina la Amrik Singh aliyezaliwa 1/2/1938 sawa na miaka (81) jijini Delhi, lakini ngozi yake haikuonyesha kama amefikia umri huo.

Baada ya kukakugiliwa na kukamtwa alipelekwa katika idara ya uhamiaji kwa kosa la udanganyifu ambapo idara hiyo imesema,

"Mipango ya Jayesh Patel ilikuwa ni kwenda Marekani kutafuta kazi, lakini 'profile' yake na udanganyifu haikumuwezesha kupata visa".