Ijumaa , 1st Feb , 2019

Raia mmoja nchini Urusi, Boris Kondrashin mwenye umri wa miaka 35, amekamatwa na polisi akijifanya daktari, baada ya kubainika kufanya tukio la mauji miaka 20 iliyopita, na kunywa damu ya mtu aliyemuua.

Boris alikamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wakazi wa mji wa Chelyabinsk nchini humo, mara tu walipomkumbuka na kukumbuka yale aliyoyafanya miaka ya nyuma.

Boris ambaye ni mtoto kutoka familia yenye heshima nchini humo huku baba yake akiwa ni mtaalamu wa masuala ya saikolojia, alitumia pesa zake kupata vyeti feki na kujifanya daktari wa saikolojia na daktari wa matatizo ya uraibu (adiction), ambapo alifanikiwa kupata kazi katika hospitali mbali mbali katika mji wa Chelyabinsk.

Mwaka 1998 kijana huyo alipokuwa mwanafunzi, alimuua mwanafunzi mwenzake na kumkatakata, kisha kula sehemu za mwili wake ikiwemo ini, na kunywa damu yake.

Polisi walipomkamata alikiri kufanya kosa hilo akijifananisha na 'vampire', na kwamba alitumwa na shetani kukamilisha kazi hiyo.

Hata hivyo mahakama ilimkuta kijana huyo na matatizo ya akili, hivyo alipelekwa kwenye kituo cha magonjwa ya akili, na alipopata unafuu aliachiwa huru.

Wakazi wa maeneo hayo wamesema kwamba walimtambua baada ya mwanamke mmoja kwenda hospitali hapo kupata matibabu. Mwanaume huyo amesema alimkumbuka daktari huyo kuwa ndiye aliyemwambia kuwa yuko kwenye orodha ya wanafunzi wengine ambao alipanga kuwaua na kuwanywa damu zao.

Boris Kondrashin