Ben Pol atoa ahadi kwa watakaochangia Namthamini

Jumamosi , 8th Jun , 2019

Msanii wa Bongofleva Ben Pol, ametoa mchango wake wa awali kwenye Kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na East Africa Television LTD.

Msanii Ben Pol akitoa maelezo

Kupitia harambee iliyofanyika Mlimani City leo Juni 8, 2019, Ben Pol ametoa taulo za kike na kuahidi atatoa tena kwa kushirikiana na wadau wake.

"Ijumaa wiki ijayo nitakuwa kwenye Friday Night Live ya East Africa Television na nitachangia lakini kwa wadau wangu wote naomba waniunge mkono na mimi nitawarusha kwenye TV siku hiyo" - amesema BenPol.

Kampeni ya Namthamini inaendelea mpaka Juni 16 ambapo itafikia kilele. Kwasasa wadau wanaendelea kukaribishwa kuchangia kampeni hiyo inayomwezesha msichana kupata taulo za kike na kusoma bila kupitia changamoto ya hedhi awapo masomoni.

Unaweza kuchangia kampeni ya Namthamini kwa kuleta mahitaji kama taulo za kike (Pedi) moja kwa moja ofisini EATV. Pili ni kwa kutuma pesa katika akaunti ya Namthamini - CRDB/ 0150431938200 au kwa Airtel Money namba - 0787 633 313 East Africa Television.