Jumanne , 11th Jun , 2024

Baada ya kampuni ya ''Apple inc'' kuchukua uamuzi wa kuungana na kampuni ya ''OpenAI'' ambao ndiyo wamiliki wa ''ChatGPT'' ili kuwezesha akili mnemba kwenye vifaa vya Apple.

 

 

Mapya yameibuka ikiwemo Elon Musk kupinga uamuzi huo na kudai kuwa ni ukiukaji wa usalama usiokubalika

''Ni jambo la kipuuzi kwamba kampuni ya  Apple haina uwezo wa kutengeneza akili mnemba ya kwao wenyewe, lakini inawahakikishia watumiaji wake usalama wa taarifa zao watakapo tumia mfumo wao'' aliandika Elon Musk

Unaweza kujiuliza kwa nini kasema hivi?

Ilivyo kwa hivi sasa Apple inc wako na mfumo unaofahamika kama SIRI ule ambao unauliza na unakupatia majibu kama Google kwa kiasi fulani, Sasa Apple kuungana na ChatGPT ni kwa lengo la kuongezea nguvu mfumo wao wa SIRI 

Hii imeonekana kuwa hatarishi kwa Bilionea Elon kwani hofu yake ni kuhusu usalama wa data za watumiaji wa bidhaa za Apple ikiwa kama mfumo wa OpenAI unaingilia taarifa za mtumiaji

Mfano kupitia Apple intelligence mtumiaji anaweza kuliza kuhusiana na ratiba yake ya kesho ikoje na akapewa jibu, kwa njia ya mfumo wa SIRI na hii ndiyo sababu Elon akasema usalama wa mtumiaji wa mfumo huu ni mdogo zaidi

Uamuzi wa sasa wa Bilionea Elon ni kuzuia vifaa vyote vya Apple inc kwenye kampuni yake ikiwemo Tesla, Space X pamoja na X ambayo awali ilikuwa ikifahamika kama Twitter ikiwa kama mfumo wao wa Apple Intelligence utaanza kutumika kwenye bidhaa za Apple

Apple Intelligence siyo akili mnemba ya kwanza kwenye kampuni za simu kwani utakumbuka ndani ya mwaka huu Samsung wenyewe walitambulisha Galaxy AI mfumo wa akili mnemba unaofanya kazi kwenye matoleo mapya ya Samsung ambayo ni S24, S24+ na S24 Ultra lakini kwa hii Apple Intelligence yenyewe itafanya kazi kwenye iOS 18, iPadOS 18, na macOS Sequoia hivyo ili kuipata itakuhitaji ku-update iOS yako.