Emmanuel Mbasha kuhusu kumuoa Muna Love

Jumamosi , 8th Feb , 2020

Msanii wa Injili Emmanuel Mbasha, amewajia juu watu ambao wanamuuliza kuhusu hatma ya Muna Love ambaye taarifa zinasema ameolewa na kubadili dini kuwa muislam na video zinamuonyesha akifunga ndoa ya kiislam.

Kushoto pichani ni Emmanuel Mbasha, kulia ni Muna Love

Taarifa hizo za kuolewa na kubadilisha dini zilisambaa zaidi siku ya jana Februari 7,2020  kupitia mitandao ya kijamii, baada ya Muna Love kuomba kupumzika kutumia mtandao wa Instagram kwa muda.

Kwa Upande wa Emmanuel Mbasha amefanunua zaidi juu ya suala hilo na ametaka watu wamkome kumuuliza kwa sababu sio mume wake na anachojua kuwa Muna ni mpambanaji wa Yesu na mfanyabiashara.

"Jamani nawaomba sana naona simu nyingi na message kuhusu kutaka  interview, nasema mimi sio mme wa Muna mnikome kama anaolewa nifanyeje sasa, ninachokujua kuwa Muna ni kamanda wa Yesu, mpambanaji, na mfanyabiashara. Huko ana-shoot filamu yake, msinisumbue  nazima simu imekua kero msinisumbue mpigieni mwenyewe" ameandika Emmanuel Mbasha