Jumatano , 4th Sep , 2019

Mtandao wa Facebook ambao ni wamiliki pia wa Instagram na WhatsApp huenda wakaja na mpango kama ambao unaendelea kufanyiwa majaribio Instagram wa kuficha uwezo wa mtu kuona 'Likes'.

Picha ya mfano wa Likes za Facebook

Tangu mwezi Julai uwezo huo ulianza kufanyiwa majaribio Instagram katika nchi kadhaa, na taarifa zinaonesha kupokelewa vizuri na watu lakini bado haujafanywa rasmi kwa watumiaji wote duniani.

Taarifa ya hivi karibuni ni kuwa mpango huo pia unaweza ukahamia Facebook, ambapo mtu atakuwa ana uwezo wa kuona idadi ya watu waliotoa Komenti lakini hawezi kuona idadi ya 'Likes' na uwezo huo utabakia kwa mtumiaji mwenyewe aliyeweka Post ndiyo atakuwa anaona idadi ya watu walio 'Like'.

Sababu za kutaka kuleta mabadiliko hayo zinatajwa ni kuweka umakini zaidi kwa watu kutazama kile kinachoandikwa kuliko picha, na kuondoa hali ya mtu kujisikia vibaya hasa pale mtu Post yake inapoonekana kushindwa kufanya vizuri.

Lakini mpango huo umekosolewa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya teknolojia, kwamba ni janja ya Facebook kutaka kujiongezea mapato zaidi.