Faiza Ally apata mrithi wa Sugu

Jumamosi , 8th Feb , 2020

Aliyekuwa mpenzi wa zamani na mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini Mr II Sugu, aitwaye Faiza Ally ameashiria kupata mpenzi mpya baada ya kupost picha akiwa naye katika mtandao wa Instgram. 

Pichani kushoto ni Faiza Ally, kulia akiwa na mpenzi wake mpya

Faiza Ally ameeleza kuwa mwanaume huyo ni baba watoto wake na ana umri wa miaka 51 au 52, na tabia yake ya  kuvaa hereni ni swaga za marekani kwa hiyo watu wasishtuke.

"Ana miaka 51 anaelekea 52 angewahi kuzaa ningekua binti yake wa kwanza, hereni isiwatishe ni swaga tu za kimarekani sio mzaramu wala mrugulu msishtuke,  kwao kawaida sana msikariri maisha, wanao hisi ni mariooo, ni hivi hali changu sili chake burudani tu wakati mwingine tuna share pia bili ili twende sawa , ndiyo utamaduni wao" ameandika Faiza Ally

Faiza Ally amewahi kusema moja kitu ambacho kimemuumiza sana katika maisha yake ni pale mpenzi wake wa zamani Mr II Sugu, alipofunga ndoa na mwanamke mwingine mwezi wa 8 mwaka 2019.