Jumatatu , 30th Oct , 2023

Kutokana na kasi ya maendeleo ya akili mnepe (A.I) kwa sasa mtandaoni, kumekuwako na uwepo wa picha nyingi ambazo zimejawa na taarifa za uongo. (za kutengeneza)

 

Google kwa sasa wamepanga kuja na programu maalumu ambayo itamuwezesha mtumiaji wa mitandao kuweza kubaini 

a) Kama picha hiyo ni yenye uhalisia (si ya kutengeneza)

b) Historia ya picha hiyo ikijumuisha siku iliyotengenezwa.

c) Wavuti ambazo zimetumia picha hizo/hiyo

d) watu wengine wametoa taarifa gani kuhusiana na picha hiyo/hizo

 

Baadhi ya wavuti ambazo zimekuwa zikitumika kwenye utengenezaji wa picha zisizo na uhalisia ni pamoja na Firefly, Midjourney,Nightcafe,Dreamstudio na nyinginezo.

 

Picha: BDM chanzo: techcrunch