Alhamisi , 13th Feb , 2020

Kampuni ya Google imetangaza kutoa kiasi cha Dola Milioni 1, sawa Tsh Bilioni mbili kwa mtu yeyote kutoka Bara la Africa atakayetoa wazo la kibunifu kuhusu usalama wa matumizi ya internet.

Picha ya mtandao wa Google

Kampuni ya mtandao huo imesema kuwa wanajua Africa kuna watumiaji wengi wa internet hivyo wanataka kijana yeyote kutoka Africa, ambaye ataweza kuleta mawazo kuhusu utoaji wa taarifa na kuboresha usalama wa faragha kwa watumiaji wake kama picha, video, na sauti.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio mjasiriamali wa teknolojia John Haule, amesema.

"Google watatoa tarehe maalum ya kutuma maombi na mwisho wa kutuma maombi hayo, atakayefanikiwa kutuma mawazo mazuri yatafanyiwa kazi na atakayeshinda atakabidhiwa kiasi hicho cha pesa" amesema Haule.

Aidha kwa upande wa mtandao wa Google wenyewe wamesema "Tunataka kuifanya internet iwe ya kushangaza na kutoa msaaada kwa watoto wa baadaye kuwa werevu kwa kutumia mbinu ya kuchambua, kutathmini  habari zao na kuchukua tahadhari kwa vyombo vya habari ili kulinda na kutunza mambo binafsi"

Google ni mtandao unaojitegemea ambao unamiliki mitandao mongine kama Youtube, G-mail na Google Chrome.