Hamisa Mobetto atuhumiwa kukwapua 'mume' wa mtu

Jumamosi , 19th Jan , 2019

Mwanamitindo na mwanamuziki chipukizi Bongo, Hamisa Mobetto, ameshushiwa tuhuma za kukwapua bwana wa mwanamitindo mwenzake, anayejulikana kwa jina la Tahiya.

Ugomvi huo ambao upo mtandaoni umeanza baada ya Tahiya kumchimba mkwara Hamisa Mobetto kuwa aachane na mpenzi wake na kuibua vita kali ya maneno baina ya wawili hao.

Hata hivyo Tahiya ameweka wazi kuamua kumuachia mwanaume huyo Hamisa Mobetto, huku vita ya maneno ikiwa inaendelea baina ya walimbwende hao kwenye runinga na mitandao ya kibongo.

Mwanamitindo Tahiya anayemtuhumu Hamisa Mobetto kumkwapua bwana wake