Hifadhi yatoa ofa ya mende 'Valentine Day'

Jumatatu , 10th Feb , 2020

Maafisa wa kituo cha maonesho ya wanyama cha San Antonio nchini Marekani wametoa ofa kwa mwenye Dola 5 sawa na Sh. 11,550, atapewa Mende ampatie jina la mpenzi wake wa zamani (Ex) na kisha kumlisha mnyama yoyote kwenye siku ya wapendanao 'Valentine Day'.

Mende na Ua la Valentine

Tukio hilo limepewa jina la "Cry Me a Cockroach" ikimaanisha 'ning'ate mimi Mende' ambapo wataruhusiwa hata wale ambao wapenzi wao wa zamani hawaishi Jijini Texas na Marekani kwa ujumla.

Kwa wale ambao wapenzi wao wa zamani walikuwa ni wabaya zaidi kwao au wakatili, watatakiwa kulipia Dola 20 sawa na Sh. 46,206 ili kupewa panya na kuwapa majina ya wapenzi wao wa zamani kisha kuwalisha wanyama.

Hiyo itakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa kituo hicho kufanya tukio la aina hiyo ambalo limezua hisia za mshangao na kuvutia kwa watu mbalimbali.