Jumatatu , 27th Jun , 2022

Kutoa ni moyo na si utajiri, na Dkt Ibrahimu Ibrahimu kutoka hospitali ya Sekou Toure, Mwanza anaishi katika maneno hayo kwa kuchangia taulo za kike pakiti 16 zitakazosaidia wanafunzi wawili shuleni kwa mwaka mzima.

Dkt Ibrahimu Ibrahimu akikabidhi taulo za kike Kwa Mratibu wa Kampeni ya Namthamini, Evelyne Ngalo.

Dkt Ibrahimu anasema wanafunzi wa vijijini ndiyo wahanga wakubwa na wanahitaji kusaidia taulo za kike kutokana na kule mazingira yao ni tofauti na mjini ambapo kuna changamoto ya upatikanaji wa taulo za kike.