Lyyn aeleza sababu ya watu kumuona mdangaji

Alhamisi , 14th Mei , 2020

Mrembo ambaye ni msanii na mwanamitindo Official Lyyn, amesema watu wanamsema kwamba anaringa, anaishi maisha ya gharama na kuonekana anadanga kwa sababu watu hawamjui vizuri.

Picha ya mrembo Official Lyyn

Akieleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, Official Lyyn amesema  "Mimi naishi maisha ya kawaida kabisa, kwenda hotelini au kula kwenye migahawa ni vitu vya kawaida, wananisema kwamba ninaringa na kujifanya mzuri ila wanasema hivyo kwa sababu hawanijui na hawajawahi kupiga stori na mimi".

"Mtu anakuwa hakujui ndiyo maana anaweza akasema vitu vingi, kama hivyo kuniambia mimi nadanga vitu ambavyo sio vya ukweli, mara nyingi safari zangu ni kwa ajili ya kazi na sio kila kitu unachofanya lazima uwaelezee watu".