Ijumaa , 28th Mei , 2021

Leo Mei 28 ni siku ya Hedhi Duniani ambapo East Africa TV na East Africa Radio imezindua Kampeni yake ya Namthamini ambayo itasaidia kutoa taulo za kike Elfu 5 kwa watoto wa kike wenye uhitaji hapa nchini Tanzania.

Picha ya msanii Madee

Katika kampeni hiyo iliyofanyika leo imezinduliwa na watu maarufu na wasanii kama Madee, Mwasiti, Chris Mauki na Devotha David ambaye ameanza kwa kutoa box saba zenye taulo za kike (pedi). 

"Mwaka jana nilisafiri na mwanangu wa kwanza ambaye yupo Form One, tulifika sehemu kula na kunywa vinywaji, wakati tumekaa kuna mdada akanifuata kuniomba mtoto wangu, akamchukua na kuelekea Toilet, baadae akatoka kuniuliza nina elfu 5" 

"Nikamuuliza ya nini akasema anataka kununua kifaa, Yeye mwenyewe aliogopa kuniambia nikampa ile pesa ila tayaru nilikuwa nimeanza kuhisi kitu, baadae akaniambia kwamba mwanangu amejichafua"

"Nilivyorudi nikamuacha kwa mama yake ili aongee nae kwamba amejichafua, baadae mama yake akanipigia simu huku analia kwamba mtoto amekuwa na amevunja ungo, nikamuuliza sasa kama wewe unalia yeye itakuaje" ameeleza Madee 

Katika kampeni hiyo iliyofanyika leo imezinduliwa na watu maarufu na wasanii kama Madee, Mwasiti, Chris Mauki na Devotha David ambaye ameanza kwa kutoa box saba zenye taulo za kike (pedi).