Alhamisi , 21st Apr , 2022

Siku kama ya leo miaka 96 iliyopita April 21, 1926 alizaliwa Malkia wa Uingereza, Malkia Elizabeth II ambaye amekua Malkia wa taifa hilo tangu Februari 6, 1952 akiwa na umri wa miaka 25.

Malkia Elizabeth akiwa na farasi wake wawili Bybeck Katie na Bybeck Nightingale.

Malkia Elizabeth atasherekehea siku yake ya kuzaliwa katika eneo maarufu la Sandringham, eneo ambalo lipo umbali wa maili 100 kutoka ikulu ya Buckingham.

Malkia ameenda kusherehekea huko siku yake kuzaliwa kwa sababu sehemu hiyo ilikuwa inapendwa sana marehemu mumewe Prince Philip aliyefariki April 9, 2021.

Usiku wa kuamkia leo iliachiwa picha ya Malkia Elizabeth akiwa na farasi wake wawili Bybeck Katie na Bybeck Nightingale.