Mtu mfupi kutoka Tanzania aweka rekodi Duniani

Ijumaa , 7th Feb , 2020

Masoud Hussein kutoka mkoani Arusha, ameingia kwenye rekodi ya Dunia kwa kuwa mtu mfupi zaidi kupanda Mlima Kilimanjaro, katika kitabu cha rekodi maarufu zaidi duniani kijulikanacho kama Guinness World Records.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Masaoud Hussein

Masoud Juma alikuwa mgeni wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla, ambaye amesema ametumia muda wake wa kumpa mchango wa senti, mawazo, mbinu, na siri ya mafanikio ili afanikishe misheni yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram,  Hamisi Kigwangalla ameeleza kuwa,

"Huyu ndugu niliyenaye hapa ni mgeni wangu bungeni leo, anaitwa Masoud Juma Hussein, wa Arusha ameingia kwenye "quest" ya kuweka rekodi ya kuwa mtu mfupi zaidi duniani kupanda Mlima Kilimanjaro, ameisajili azma hii kwenye kitabu cha rekodi maarufu zaidi duniani kijulikanacho kama Guinness World Records, tumuombee kheri" ameandika.