Jumamosi , 9th Feb , 2019

Mwanamke mmoja nchini Urusi ameuawa na nguruwe aliokuwa anawafuga baada ya kuanguka kwenye banda la wanyama hao.

Picha ya Nguruwe.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Urusi, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 56 alikuwa akiwalisha nguruwe ndipo ghafla akaanguka na nguruwe hao wakamtafuna, inasadikiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwake ilikuwa ni kuzirai ama kupatwa na kifafa.

Tukio hilo limeripotiwa kwenye wilaya Malopurginsky jimboni Udmurtia, lililopo katikati ya Urusi ambapo mume wa marehemu alikuwa amelala wakati mkewe alipokuwa akiwahudumia nguruwe hao. Baada ya kuamka alianza kumtafuta mkewe na kukuta mwili wake ndani ya banda la nguruwe.

Oktoba mwaka 2012 tukio kama hilo liliripoptiwa nchini Marekani katika jimbo la Oregon. Bwana Terry Vance Garner, aliyekuwa na miaka 69 wakati huo alienda kuwalisha nguruwe wake lakini hakurejea.