"Nitazaa hadi itakaposhindikana" - Tausi Mdegela

Alhamisi , 4th Jun , 2020

Msanii wa filamu ambaye ni mzazi wa mtoto mmoja wa kike, Tausi Mdegela amesema mwanaye huyo anamkataa na anampenda sana baba yake kuliko yeye, pia ana mipango ya kuzaa mpaka pale itakaposhindikana.

Msanii wa filamu Tausi Mdegela akiwa na mtoto wake wa kike

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Tausi Mdegela amesema, mwanaye anaendelea vizuri na muda wote yupo naye.

"Raha sana kuwa na kitu unachokitegemea halafu ukakipata, kwa sababu mtoto unaanza kuongea naye tangu yupo tumboni, ila mwanangu ananikataa sana ana-enjoy akiwa na baba yake, anaweza akawa ananyonya ila akishafika baba yake anaacha anakuwa na furaha kisha anacheka kwa nguvu" amesema Tausi

Aidha ameendelea kusema  "Siwezi nikataja nataka watoto wangapi ila huyu akikua atapata mdogo wake na ndugu zake watafuata, pia siwezi nikasema nipate watoto wangapi maana itategemea uhai na mipango ya Mungu ila nitazaa mpaka pale itakaposhindikana".

Zaidi tazama akiongea kwenye video hapa chini.