Ijumaa , 26th Sep , 2025

Ni siku 90 zimebakia kuelekea sikukuu ya Christmas na siku 96 zimebakia kumaliza mwaka 2025.
Tunapokaribia mwisho wa mwaka, ni wakati mzuri wa kutazama tulipotoka. Ukiangalia akiba na mipango yako, hivi ni baadhi ya vitu muhimu vya kujikumbusha:

1. USHINDI NI HATUA, SIO KIASI: Haijalishi umefikisha kiasi gani, jipongeze kwa kila shilingi uliyoweza kuweka kando. Safari ya mafanikio hujengwa kwa hatua ndogo ndogo za nidhamu. Upo mbali zaidi ya ulipokuwa Januari.

2. HUJACHELEWA BADO: Siku 98 zilizobaki ni fursa kubwa Bado unaweza kuanza kuweka akiba, kukamilisha lengo dogo, au kupanga upya mikakati yako. Muhimu sio kuanguka, bali kuinuka na kuendelea. Anza leo.

3. AKIBA SI PESA TU: Tazama pia akiba yako ya kiafya, kielimu, na mahusiano. Je, umejifunza kitu kipya? Umeimarisha afya yako? Umejenga urafiki mpya? Hizi nazo ni hazina kubwa.

4. MAFUNZO YA MWAKA: Kila changamoto ya kiuchumi uliyopitia mwaka huu ni somo. Jiulize, “Nimejifunza nini kuhusu matumizi na mapato yangu?” Tumia mafunzo hayo kujipanga vizuri zaidi kwa mwaka 2026.

Swali la siku: Wewe unajivunia nini zaidi ulipofanikiwa mwaka huu, kifedha au maeneo mengine ya maisha? Tuambie kwenye comments.