Yesu feki aliyetembelea Kenya adaiwa kufariki

Jumanne , 6th Aug , 2019

Michael Job raia wa Marekani ambaye ni mhubiri na muigizaji anayeidaiwa kuwa Yesu Feki, ameripotiwa kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali moja nchini Kenya.

Michael Job akiwa anaongea nchini Kenya.

Hospitali moja nchini Kenya ya Heyn inaelezwa kutoa taarifa za Michael Job kufika kwaajili ya matibabu na kisha kufariki hospitalini hapo. Imeeleza kuwa alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na amefariki wakati akipatiwa matibabu.

Yesu feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita na alikuwa mgeni katika siku ya tamasha la dini ya wakristo nchini humo na kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi.

Picha na Video zilimuonyesha Michael Job akiwa amevalia mavazi kama ya Yesu wa ukweli zilienea kwa wingi katika mitandao ya kijamii hasa barani Africa.

Hata hivyo ukurasa wake wa mtandao wa Facebook 'Michael Job' umeendelea kupandisha picha na video ukimwonesha akitoa mahubiri kama inavyoonekana hapo chini.