Alhamisi , 27th Jan , 2022

Michuano yamataifa ya Afrika ‘AFCON’ imefikia michezo ya mtoano hatua ya robo fainali baada ya michezo ya hatua ya 16 kutamatika usiku wa jana Januari 26, 2022.

(Egpyt wakishangilia kufuzu Robo fainali na Timu ya Senegal)

Mabingwa watetezi, Mafarao wa Misri wamepata ushindi wa penalty 5-4 dhidi ya Ivory Coast ‘Tembo wa Afrika’ baada ya sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120. Erivk Baily alikosa penalti kwa Ivory Coast na MO Salah akaivusha Egypt.

Kwa upande mwingine, Mali aliondoshwa kwenye hatua hiyo baada ya kufungwa kwa penalty 6-5 dhidi ya Equtorial Guinea kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 na zile 30 za niongeza.

Kwa matokeo hayo, Mabingwa wa Kihistoria Misri watacheza na Mabingwa wa CHAN, timu ya taifa ya Morocco ilhali Equatorial Guinea ikipangwa kucheza na Senegal Jumapili ya Januari 30, 2022.

Gambia ambayo inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza, imetinga hatua ya Robo fainali kwa mara ya kwanza na itacheza dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo timu ya Cameroon wakati Burkina Faso itacheza na Tunisia Januari 29, 2022.