Jumanne , 21st Sep , 2021

Wachezaji wapya wakimataifa wa Yanga, Khalid Aucho, Fiston Mayele na Djuma Shaban, ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kucheza mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Simba Siku ya Jumamosi Septema 2021 baada ya kukosa michezo miwili ya kuwania kufuzu ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United.

(Wachezaji wapya wa Yanga, mlinzi wa kulia, Djuma Shabani (kushoto), Kiungo Khalid Aucho (katikati) na mshambuliaji Fiston Mayele (kulia) walioshindwa kucheza michezo miwili ya kufuzu makundi klabu bingwa Afrika dhidi ya Rivers United baada ya vibali vya vya kimataifa kuchelewa.)

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari za michezo siku ya leo Septemba 2021 ndani ya makao makuu ya TFF akiwa pamoja na Kaimu Afisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga.

Pia Bumbuli amewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kuwa hakuna mchezaji yoyote mwenye majeraha kuelekea mtanange huo wa kukata na shoka utakaopigwa kwenye dimba la Mkapa.

Kwa upande wa mabingwa wa Kabumbu nchini Tanzania bara, Simba watakuwa wenyeji wa mchezo huo ambapo Kamwaga amesema kuwa wachezaji wote wapo salama na hakuna mwenye majeraha kuelekea mchezo huo.

Pia Kamwaga ametoa salamu za pongezi kwa Azam FC na Biashara United baada ya kufanikiwa kuvuka hatua ya pili ya mashindano ya  kombe la shirikisho  baranai Afrika, huku akitoa nasaha ya kuzilinda nafasi hizo.