
Mshambuliaji wa Azam FC Ayoub Lyanga amefunga mabao yote mawili ya ushindi leo.
Mabao yote mawili ya Azam FC kwenye mchezo huu yamefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 20 na 54 na lile la Mtibwa Sugar limefungwa na Hamisi Ndemla dakika ya 80 ya mchezo. Kwa ushindi huu Azam FC imefikisha alama 36 na wamepanda kutoka nafasi ya 5 hadi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi.
Mtibwa Sugar wamesalia nafasi ya 10 na alama zao 28 na huu ni mchezo wa 3 mfululizo wamecheza bila kupata matokeo ya ushindi wamefungwa michezo 2 na sare mchezo mmoja. Wanatofautiana alama 2 na Ruvu Shooting walio kwenye mstari wa kushuka daraja wenye alama 26.
Mchezo wa mwisho wa Ligi kuu leo unachezwa Saa 3:00 Usiku ambapo klabu ya Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting, mchezo huu unachezwa uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.