.jpg?itok=3n02ml_9×tamp=1661785754)
Kocha Mkuu Hamid Moalin na Msaidizi wake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na klabu hiyo zilisema makocha hao wataendelea kusalia ndani ya timu hiyo kama sehemu ya idara ya ufundi katika nafasi nyingine watakazozitangaza baadaye.
Taarifa hiyo ilisema kwa sasa, timu itakuwa chini ya kocha wa makipa Daniel Cadena.
"Tumefikia makubaliano ya pande mbili kwa kocha wetu mkuu na msaidizi kuachia ngazi katika nafasi hizo na kocha mpya tutamtangaza baadaye." ilisema taarifa hiyo.
Moallin alipewa majukumu ya kukinoa kikosi hicho tangu msimu uliyoisha, akiziba nafasi ya George Lwandamina, ambapo msimu huu (2022/23) alikiongoza kikosi hicho katika mechi dhidi ya Kagera Sugar waliyoichapa mabao 2-1 na Geita Gold ambapo walimaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.