Azam yafanya kweli kwa Niyonzima

Jumamosi , 1st Aug , 2020

Klabu ya Azam Fc imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo Ally Niyonzima kutoka Rayon Sports ya Rwanda kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

Kiungo Ally Niyonzima raia wa Rwanda (Kulia) akisaini mkataba wa miaka miwili mbele ya ,Mtendaji Mkuu wa Azam Fc Abdulkarim Amin.

Kupitia mitandao ya kijamii ya Klabu hiyo, imeelezwa kwamba huo ni usajiliĀ  uliotokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha mkuu wake Aristica Cioba.

Niyonzima ambaye yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda Amavubi anakua mchezaji wa pili kufuatia usajili wa kiungo Awesu Awesu kutoka Kagera Sugar.