Alhamisi , 13th Aug , 2020

Klabu ya Azam Fc ya Jijini Dar es salaam imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja nyota wake Idd Seleman (Nado) ili kuendelea kusalia mitaa ya Chamazi hadi mwaka 2020.

Winga machachari wa Azam Fc Idd Seleman (Pichani) akikokota mpira katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya KMC .

Mkataba wa awali wa nyota huyo ulikua umalizike mwaka 2021,ini kutokana na kiwango na mchango wake , Azam imeamua kumuongezea mkataba huo aendelee kuitumikia miamba hiyo inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

Winga huyo alisajiliwa Azam mwaka jana ikitokea Mbeya City ambako katika msimu juzi alifunga mabao kumi kiasi cha kumvutia aliyekua kocha wa wana lambalamba ,Etienne Ndayiragije

Nado amefanikiwa kufunga mabao tisa katika mashindano yote kwenye msimu uliomalizika,saba kati yao ni ya Ligi Kuu na mawili kwenye Kagame Cup yaliyofanyika nchini Rwanda Mwaka jana.