Jumatatu , 31st Dec , 2018

Aliyekuwa kocha wa Mbao FC Amri Said amejiunga na Biashara United ya Mara wiki chache tangu aachane na Mbao ya Mwanza.

Kocha Amri Said

Uongozi wa klabu ya Biashara United umethibitisha kuwa Amri Said Stam amekuwa kocha mkuu wa timu hiyo akichukua nafasi ya Hitimana Thiery aliyefutwa kazi kutokana na matokeo mabaya.

Kwa upande wake kocha Hitimiana Thiery tayari ameshapata kibarua cha kuwa kocha mkuu wa timu ya Namungo inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Biashara United wanajiandaa na mchezo wa ligi kuu Jumatano hii ya tarehe 3, ambapo watakuwa nyumbani dhidi ya Mbeya City ya mkoani Mbeya.

Amri Said aliachana na Mbao FC baada ya wabishi hao wa Mwanza kumleta kocha Ali Bushiri awe msadizi wa wake jambo ambalo hakukubaliana nalo kutokana na wote kuwa na leseni B ya ukocha hivyo akaamua kuondoka.