Jumanne , 4th Jun , 2019

Baada ya shirikisho la soka nchini (TFF), kuthibitisha kuwa Tanzania imepewa ruhusa ya kuingiza timu 4 kwenye michuano ya vilabu Afrika, klabu ya Simba imetoa ujumbe.

Wachezaji wa Simba

Kwa mujibu wa TFF, ni kwamba shirikisho la soka Afrika limewathibitishia kuwa pointi ambazo zimepatikana katika miaka 5 iliyopita zimesaidia nchi kuongezewa timu mbili hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa zitakwenda Simba na Yanga huku shirikisho zikienda Azam FC na KMC.

Simba wameweka ujumbe kwenye mtandao wa Instagram, ikionesha kumbukumbu ya siku walipoitoa AS Vita na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

''Ilikuwa siku ya kihistoria kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuongeza alama ambazo zimeiwezesha nchi yetu kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa msimu wa 2019/2020''.
 
Ujumbe huo umemalizika kwa maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa ambayo ni ''SIMBA IKISHINDA, TANZANIA IMESHINDA.