Alhamisi , 18th Feb , 2016

Baba mzazi wa mshambuliaji wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa,Edison Cavan,amesema anataka mwanae aondoke ndani ya klabu hiyo na akajiunge na vilabu vya Manchester United,Real Madrid au Juventus.

Hatua hiyo inakuja kutokana na madai kuwa mwanaye haanzishwi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Ufaransa.

Luis Cavan Akiieleza Televisheni ya Israel Sport 5, amesema "Zlatan hataki kucheza pembeni,..kwahiyo wanamkwaza Edinson Edison anataabika PSG, kama wakimwacha acheze namba 9 atafurahia.... Ningependa kumwona akichezea Real Madrid, Manchester United au Juventus".

Cavan alifunga bao la ushindi la PSG kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea Jumanne akitokea benchi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.

Cavan alijiunga na PSG akitokea klabu ya Napoli kwa dau la paundi milioni 55 mwaka 2013 na hadi sasa amebakiza miaka 2 kwenye mkataba wake.