Jumatatu , 18th Mar , 2019

Uongozi wa Simba umetangaza masikitiko yake kufuatia kifo cha shabiki wake maarufu mkoani Rukwa wakati wa mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club.

Kushoto ni kiungo wa Simba, Clatous Chama na kulia ni shabiki aliyepoteza maisha, Peter Kitili.

Kupitia kurasa za kijamii za Simba, imeelezwa kuwa kifo cha shabiki huyo aliyejulikana kwa jina la Peter Kitili, kimetokea wilaya ya Mpanda mkoani humo ambapo amepoteza maisha alipokuwa akishangilia ushindi.

 

Shangwe kubwa la mashabiki wa Simba liliibuka baada ya kiungo, Clatous Chama kuhitimisha kalamu ya bao la 2 kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Vita katika uwanja wa taifa, wikiendi iliyopita.

Simba sasa imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, ikiwa ni hatua kubwa zaidi kufikiwa na klabu za Tanzania katika miaka ya karibuni tangu mwaka 1974 ambapo Simba ilifikia hatua hiyo.