Jumamosi , 5th Oct , 2019

Katika vitu ambavyo vilikuwa vya kusisimu katika fainali ya kwanza ni namna mastaa, Baraka Sadick wa Mchenga na Baraka Mopele wa Tamaduni, walivyochuana kuzipambania timu zao.

Moja ya matukio katika game 1

Baraka Sadick aliibuka mfungaji bora wa mchezo kwa kufunga pointi 47, Rebounds 3 na Assist 3 huku Baraka Mopele akifunga jumla ya pointi 21, Rebound 1 na Assist 1, akizidiwa na mchezaji Stephano Mshana aliyeongoza kufunga pointi nyingi kwa upande wa Tamaduni, akifunga pointi 37, Rebounds 7 na Assist 5.

Baraka Mopele alikutana na changamoto ya ufungaji, kwani alikosa nafasi nyingi za kufunga huku mpinzani wake Baraka Sadick akitumia vizuri nafasi kutokana na umbo lake, kasi na umakini alionao.

Kwa upande wa mastaa waliohudhuria, Country Boy alionekana kuishangilia Mchenga, hasa pale Baraka Sadick alipokuwa akifunga na Moni Centrozone akiisapoti Tamaduni ya kina Denis Chibula 'Babu' na Baraka Mopele.

Ikumbukwe kuwa Baraka Sadick ni MVP wa Sprite Bball Kings 2018 na wakati huo Baraka Mopele akiweka ahadi ya kushindana naye kwenye ubingwa na tuzo ya MVP msimu huu. Tusubiri na tuone mchuano utakavyoishia.