Barcelona ilivyofaidika na mipango ya Liverpool

Jumatano , 1st Mei , 2019

Kuelekea mchezo wa nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Barcelona dhidi ya Liverpool, kuna wachezaji 8 ambao wamechezea vilabu vyote viwili.

Wachezaji wa Barcelona

Kati ya hao wachezaji nane, wawili pekee ndio bado wanacheza na huenda wote wakawepo kwenye mchezo wa leo wakiwa upande wa Barcelona.

Wachezaji hao ni Philippe Coutinho na Luis Suarez ambao wote walicheza Liverpool, kabla ya kutimkia Barcelona kwa miaka tofauti.

Barcelona itanufaika na uwepo wa nyota hao wawili ambao walicheza kwa viwango vya juu wakiwa ndani ya Liverpool huku pia wakiwa kama nahodha wasaidizi wa kikosi hicho.

Wachezaji wengine ambao wamewahi kucheza katika timu zote mbili ni Javier Mascherano, Pepe Reina, Mauricio Pellegrino, Bolo Zenden, Jari Litmanen, Luis Garcia.