Ijumaa , 25th Feb , 2022

Klabu ya FC Barcelona imefuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Europa League kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3 dhidi ya Napoli, hii ni mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 jana usiku kwenye mchezo wa mkondo wa pili hatua ya mtoano. Na Droo ya hatua ya 16 bora inafanyika leo.

Wachezaji wa Barcelona wakishangilia kwenye mchezo dhidi ya Napoli

Mabao ya Barcelona kwenye ushindi huo yamefungwa na Jord Alba, Frank De Jong, Gerald Pique na Aubameyang, na yale ya wenyeji Napoli yamefungwa na Lorenzo Insigne na Matteo Polittano. Barca wamefuzu kwa ushindi wa ju,la wa abao 5-3 kwani mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizi zilitoka sare ya bao 1-1 mchezo uliochezwa wiki iliyopita.

Ushindi huu pia ni wa kihistoria kwa Barcelona kwani ni kwa mara ya pili wamepata ushindi wakuanzia mabao 4 katika aridhi ya Italia, mara ya mwisho kupata ushindi wa mabao 4 kwenye taifa hilo ilikuwa mwaka 1959 ambapo waliifunga Inter Milan mabao 4-2..

Lakini pia droo ya hatua ya 16 bora inafanyika leo, makao makuu ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA huko Nyon, Switzerland. Droo hiyo inahusisha timu 8 zilizomaliza vinara wa makundi ambazo ni Crvena zvezda, Eintracht Frankfurt, Galatasaray, Leverkusen, Olympique Lyon, Monaco, Spartak Moskva na West Ham.

Timu nyingine 8 ni zilezofuzu kutoka hatua ya mtoano ambazo ni Atalanta, FC Barcelona, Real Betis, Braga, RB Leipzig, FC Porto, Rangers na Sevilla.