(Wachezaji wa Bayern Munchen wakishangilia goli)
Bayern ilipata ushindi huo mnono mwaka 2012 ambapo Bayern iliifunga FC Basel ya Uswizi mabao 7-0, 7-0 tena dhidi ya Shakhtar Donestk mwaka 2015, 7-1dhidi ya Bayer Leverkusen mwaka 2012, 8-2 dhidi ya Barcelona mwaka 2020, 7-2 dhidi ya Spurs 2020 na 7-1 RB Salzburg usiku wa kuamkia leo.
Kwa ushindi huo Bayern munich imefanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali ya Michuamo hiyo huku mshambuliaji wake tegemezi, Robert Lewandowski akifunga mabao matatu 'Hat-trick' na kuweka rekodi mbalimbali za kibabe.
'Hat-trick' hiyo ni ya tano kwa Lewandowski na kuungana na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kuwa wachezaji watatu pekee kwenye historia ya Ligi hiyo kufunga 'Hat-trick' nyingi zaidi, Messi na Ronaldo wote wakiwa na 'Hat-trick' 8 kila mmoja.
Lewandowski pia amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 40 msimu huu kwenye michuano yote katika ligi tano barani Ulaya huku akiwa amecheza michezo 35 na kufunga magoli 42 na assist 4.
Naye, Mshambuliaji pacha wa Lewandowski, Thomas Muller amefikisha magoli 52 ya michuano hiyo na kuwapiku Thierry Henry, Zltana Ibrahimovic na Andriy Shevchencko baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi huo wa mabao 7-1.
Real Madrid watawakaribisha PSG ya Ufaransa wakati Manchester City wataikaribisha Sporting Lisbon ya Ureno ikiwa ni michezo miwili ya mkondo wa pili hatua ya 16 bora itakayochezwa saa tano kamili usiku wa leo.





.jpg?itok=5cvL0YaP)