
Sheikh Khaled
Mike Ashley amefikia makubaliano na Seikh Al Nehayan ya kuiuza klabu hiyo kwa pauni milioni 350 na tayari mkataba umekwishasainiwa kabla ya kupelekwa kwa uongozi wa bodi ya Ligi Kuu nchini Uingereza.
Bilionea huyo ni mmoja wa familia ya kifalme ya Abu Dhabi, ambapo msimu uliopita alifeli ofa yake ya kuinunua Liverpool kwa pauni bilioni 2.
Newcastle United imekuwa katika mipango ya kununuliwa hivi karibuni kutoka kwa Amanda Staveley na Peter Kenyon lakini ofa zao hazikufanikiwa. Baaada ya Sheikh Khaled kuinunua klabu hiyo, inaelezwa kuwa kazi yake ya kwanza itakuwa ni kumpa mkataba wa kudumu kocha Rafa Benitez.
Sheikh Khaled bin Zayed Al Nehayan ni nani?
Shaikh Khaled (61) ni mmoja wa mwanafamilia ya Emirati ambaye anaiongoza Abu Dhabi kwa sasa. Alianzisha kampuni maarufu kama 'Bin Zayed Group', inayojishughulisha na biashara za ndani na za Kimataifa mnamo mwaka 1988, ambapo hivi sasa inatambulika kama biashara kubwa zaidi katika ghuba ya Asia.
Mwezi Agosti, 2018, Sheikh Khaled alipeleka ofa ya pauni bilioni 2 iliyoweka rekodi, ambapo alitaka kuinunua klabu ya Liverpool. Sheikh Khaled ni mjomba wa mmiliki wa sasa wa klabu ya Manchester City, Sheikh Mansour bin Zayed, ambaye kabla ya kuinunua Man City mwaka 2008 alikuwa katika mazungumzo ya kuinunua klabu hiyo ya Newcastle United, mazungumzo ambayo yalifeli.