Mzamiru Yassin akishangilia bao katika moja ya mechi za ligi kuu alizoifungia Simba
Mzamiru ameifungia Simba bao pekee dhidi ya KVZ ikiwa ni dakika ya 44 baada ya kuitumia vyema kros ya Abdi Banda na kumchambua kipa wa KVZ wakati walinzi wake wakimuacha kwa kudhani kuwa alikuwa ameotea.
Bao hilo limedumu hadi mwisho wa mchezo ulioshuhudia soka la ushindani na pasi nyingi kwa pande zote licha ya Simba kukosa mabao mengi kutokana na washambuliaji wake kukosa maarifa dhidi ya uimara wa golikipa wa KVZ.
Hilo ni bao la pili kwa Mzamiru kuifungia Simba katika michuano hiyo ambapo katika ushindi wa 2-1 iliyoupata dhidi ya Taifa Jang'ombe, alifunga bao la kwanza, na katika ligi kuu Tanzania Bara tayari ana mabao sita
Katika mechi iliyopigwa mapema leo, mabingwa watetezi URA wameonja kipigo kwa kuchapwa mabao 2-1 na Jang'ombe Boys
Kwa matokeo hayo Simba wanakuwa vinara wa kundi B wakiwa na pointi 6 wakifuatiwa na URA yenye point tatu, Jang'ombe Boys point 3, Taifa Jang'ombe pia point 3 huku kvz ikiwa haina point hata moja.





