
Nahodha wa klabu ya wekundu wa Msimbazi John Bocco
Bocco ameeleza hayo baada ya dakika chache kupita tokea ulipomalizika kwa mtifuano wao dhidi ya Kagera Sugar ambapo Simba wamefanikiwa kutoka na ushindi wa bao 2-0.
"Kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kumaliza mchezo wetu wa leo salama na kupata alama 3, kiukweli Juma Kaseja ni goli kipa mzuri na ambae nina muheshimu sana", alisema Bocco.
Pamoja na hayo, Bocco aliendelea kwa kusema " mchezo ulikuwa mgumu sana katika kipindi cha kwanza kwa maana wenzetu pia walijipanga sana katika mchezo wa leo".
Matokeo ya leo yanaifanya timu ya Simba SC kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 32 katika michezo 14 na kuishusha Azam FC yenye alama 30.