Jumatatu , 17th Mar , 2014

Polisi Moro yatangulia ligi kuu

Michuano ya ligi Daraja la kwanza FDL inayoendelea hivi sasa hapa nchini ikichezwa kwa makundi mataatu ya A, B na C iko katika mzunguko wa lala salama ambako mpaka sasa ni timu ya Police Morogoro toka kundi B ndiyo timu ambayo imeshajihakikishia moja ya nafasi tatu za kupanda daraja

Afisa wa Ligi toka Bodi ya ligi Joel Balisydia amesema kutokana na ubora wa timu zinazoshiriki ligi hiyo katika makundi yote wanamatumaini timu zitakazopanda ligi kuu zitaleta ushindani mkubwa katika ligi hiyo msimu ujao.