Nyota wa Milwaukee Bucks, Brook Lopez akiwania mpira na mlinzi wa Atlanta Hawks, Kevin Huerter.
Licha ya kucheza bila nyota wake Giannis Antetokounmpo mwenye maumivu ya goti lake la kulia, lakini alikuwa Brook Lopez aliyewashangaza wengi kwa kuonesha kiwango safi kwa kufikisha alama 33 na rebaundi 7 zilizomfanya kuwa nyota wa mchezo huo mbele ya Khris Middleton.
Khris Middleton aliibuka kuwa nyota wa mchezo uliopita aliambulia alama 26, rebaundi 18 na assist 3 huku Bogdan Bogdanovic wa Atlanta licha ya kutoa upinzani mkali na kupata alama 28, rebaundi 5 na assist 4 lakini hazikutosha kuwafanya Atlanta wasim-miss Trae Young aliyeumia kifundo cha mguu.
Taarifa kutoka Hawks zinasema, baada ya nyota wake Trae Young kukosa michezo miwili kutokana na maumivu hayo, huenda nyota huyo akarejea kikosini kwenye mchezo wa mzunguko wasita pamoja na mlinzi wake Clint Capela aliyeumia jichoni baada ya kupigwa kiwiko kwenye mchezo wa mzunguko 3.
Baada ya ushindi huo, sasa Bucks wanahitaji ushindi mmoja kwenye mchezo wake unaofuata dhidi ya Atlanta utakaochezwa Julai 4 mwaka huu ili kuwa mabingwa wa NBA ukanda wa Mashariki ili kumuwezesha kutinga fainali ya NBA ya kanda zote dhidi ya mabingwa wa Magharibi, Phoenix Suns.





