Jumanne , 31st Mar , 2015

Nahodha wa Klabu ya Yanga, Nadir Haroub Canavaro amesema, hali ya hewa haiwezi kuchangia timu kufanya vibaya katika michuano mbalimbali ya ndani au nje ya nchi.

Akizungumza na East Africa Radio, Canavaro amesema, mchezaji yoyote anatakiwa kuzoea hali ya hewa iwe ya joto au baridi na kujibidiisha katika mazoezi na kuweka mawazo yake katika mchezo itamsaidia kuweza kufanya vizuri.

Canavaro amesema wachezaji wenzake wapo tayari kwa ajili ya mchezo na anaamini kila mchezaji ana uwezo wa kumuhamasisha mwenzake ili kuweza kufanya vizuri katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho watakayocheza dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe Mei 4 mwaka huu Nchini Zimbabwe.