
Clatous Chama akimkabidhi jezi shabiki wake
Taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba imeonesha picha ya mchezaji huyo akimkabidhi shabiki wake jezi yenye jina lake.
"Mchezaji wetu Clatous Chama amemkabidhi zawadi ya jezi shabiki wa timu yetu, Raphael Oleshang'ai maarufu kama Mtakatifu Jr baada ya siku kadhaa zilizopita picha yake kusambaa katika mitandao ya kijamii akimuomba Chama ampe jezi," imesema taarifa hiyo ya Simba.
Katika hatua nyingine, uongozi wa Simba umemtangaza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhe Joseph Kakunda kuwa mgeni rasmi wa mchezo wa kesho wa Klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya Nkana Red Devils ya nchini Zambia katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Simba itacheza na Nkana Red Devils kesho Jumapili Desemba 23, mchezo wa marudio baada ya kufungwa kwa mabao 2-1 nchini Zambia. Endapo Simba itaiondoa Nkana, itafanikiwa kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu 2003.