Alhamisi , 8th Mei , 2014

Chama cha netball Tanzania CHANETA kimesema bado kinatafuta fedha kwa ajili ya kuendeleleza program za mchezo huo kwa vijana hasa kuanzia mashuleni mpaka vyuoni ambako ndiko kunapatikana vijana wengi na wenye vipaji.

Mwenyekiti wa CHANETA Anna Kibira

Chama cha netball Tanzania CHANETA kimesema bado kinatafuta fedha kwa ajili ya kuendeleleza program za mchezo huo kwa vijana hasa kuanzia mashuleni mpaka vyuoni ambako ndiko kunapatikana vijana wengi na wenye vipaji.

Mwenyekiti wa CHANETA Anna Kibira amesema walishaanza mpango wa kufuatilia vijana tangu walipoingia madarakani na ndio maana waliyatumia mashindano ya shule za sekondari nchini UMISETA kusaka vipaji na walifanikiwa kupata vijana zaidi ya 80 wa umri chini ya miaka 18 ambao wataunda kikosi cha vijana kitakachoshiriki michuano ya Afrika itakayofanyika nchini Botswana mwaka huu.