(Nyota wa Phoenix Suns, Chris Paul 'CP3'.)
Chris Paul ‘CP3’ ni mchezaji muhimu zaidi kwenye tim ya Suns kwani ana uwiano mzuri wa kufunga alama 14.9, rebound 4.5 na assist 10.7 jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya wawe vinara wa Ukanda wa Magharibi.
CP3 ameisaidia Suns kuwa na matokeo mazuri sana kwani tokea January 2022 Suns imecheza michezo 23, imeshinda michezo 21 na kupoteza 2 pekee na kuwa na rekodi bora ya msimu huu ya kushinda michezo 48 na kufungwa 10 tu.
Jukumu la kuibeba Suns sasa linazidi kubaki kwa Devin Booker ambaye ndiye wanayomtegemea pia kwenye kuwafungia alama nyingi. CP3 huenda akacheza michezo ya NBA Playoffs akirejea dimbani nah ii ni endapo Suns watafuzu.





