Ripoti mbalimbali za vyombo vya habari nchini England leo zinaeleza kuwa kocha huyo raia wa Italia bado anafanya maamuzi kuhusu mstakabali wake ndani ya klabu ya Chelsea.
Wengi wameonekana kushangazwa na maamuzi hayo ya kutoa siku tatu za mapumziko kwa wachezaji ilihali timu haifanyi vizuri. Mechi iliyopita Chelsea pia ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Bournemouth.
Mabingwa hao watetezi wa EPL watarejea uwanjani siku ya ijumaa kwaajili ya kuanza maandalizi ya kuivaa West Bromwich Albion kwenye uwanja wa Stamford Bridge Jumatatu ijayo.





