Cristiano Ronaldo
Ronaldo alikuwa akiiongoza Juventus katika mchezo wa robo fainali ya kombe hilo la pili kwa ukubwa nchini Italia na wamekubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Atalanta katika mchezo wa robo fainali.
Ronaldo akiwa na Manchester United alifanikiwa kuchukua klabu bingwa Ulaya mwaka 2008 pamoja na ligi kuu ya England lakini hakufanikiwa kushinda trebble baada ya kombe la FA kuchukuliwa na Portsmouth.
Baada ya kutimkia Real Madrid mwaka 2009 Ronaldo amefanikiwa kutwaa taji la klabu bingwa mara 4 lakini mara zote hakubahatika kutwaa trebble kutokana na ubingwa wa La Liga na Copa del rey kuchukuliwa na Barcelona katika misimu hiyo.
Trebble ni nini?
Ni mujumuiko wa mataji matatu makubwa kwenye ligi ambayo yanahusika taji moja la Bara yaani klabu bingwa ya bara husika na mataji mawili ya ndani ya nchi.
Kwa mfano nchini England mataji mawili yanayotambulika kwenye trebble ni FA Cup na EPL. Hispania ni La Liga na Copa del rey. Ujerumani ni Bundesliga na DFB Pokal.
Rekodi za Trebble
Barcelona ndio timu inayoshikilia rekodi ya kushinda trebble mara mbili katika misimu ya 2008/09 na 2014/15. Manchester United pia ilitwaa msimu wa 1998/99. Inter Milan ilitwaa msimu wa 2009/10. Bayern Munich ilitwaa msimu wa 2012/13.




