Daktari wa Yanga amalizana na Kamusoko

Jumatano , 14th Feb , 2018

Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiwa majeruhi hatimaye kiungo wa Yanga Thabaani Kamusoko amerejea na anatarajiwa kucheza kweney mchezo wa ligi kuu leo dhdi ya Majimaji FC kwenye uwanja wa Uhuru.

Afisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa daktari wa timu hiyo Dr. Bavu ametoa ruhusa ya Kamusoko kutumika hivyo ni jukumu la benchi la ufundi kuamua kumchezesha kama atakuwa amefanya vizuri kwenye mazoezi.

Aidha kwa upande mwingine Dismass amesema timu hiyo itaendelea kuwakosa nyota wake wanne ambao ni Abdallah Shaibu, Donald Ngoma, Yohana Mkomola na Amisi Tambwe kutokana na kuendelea kuuguza majeraha.

Mchezo wa raundi ya kwanza kati ya Majimaji na Yanga SC uliopigwa mjini Songea, ulimalizika kwa sare ya 1-1 na leo timu zinakutana katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

Yanga kwasasa ina alama 34 katika michezo 17 ikiwa katika nafasi ya pili huku Majimaji ikiwa na alama 14 katika nafasi 14.