Jumanne , 11th Aug , 2020

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea za England Daniel Sturridge amesema anataka kucheza tena katika ligi kuu ya England EP.

Sturridge kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Trabzonspor mwezi machi

Sturridge kwa sasa hana timu toka mwezi machi baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Trabzonspor ya Uturuki. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alivunja mkatab na timu hiyo baada ya kufungiwa miezi minne na shirikisho la soka la England FA baada ya kujihusisha na mchezo wa kubashiri yani betting ambapo kikanunu wachezaji hawaruhusi kujiusisha na mchezo huo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England amesema kipindi hiki anachosikiliza ofa za usajili kutoka katika timu tofauti tofauti kutoka ligi mbali mbali ulaya atazipa zaidi kipaumbele timu za ligi kuu England EPL.

Sturridge ameshawahi kuvitumkia vilabu kadhaa vya EPL ambavyo ni Manchester city, Chelsea, Bolton Wanderers, Liverpool na West Bromwich Albion, na ameshinda ubingwa wa ligi kuu England EPL na wa ligi ya mabingwa ulaya Uefa Champions League akiwa na Chelsea anaamini uzoefu wake kwenye timu kubwa utambeba zaidi na bado anauwezo wa kucheza katika ligi hiyo tajiri duniani