
Welbeck, 25, aliumia goti lake la mguu wa kulia kwenye mchezo wa timu yake uliosha kwa sare ya 2-2 na Manchester City jumapili iliyopita, hivyo anatarajiwa kukosa michuano ya Mataifa ya Ulaya mwezi ujao nchini Ufaransa.
Klabu yake imesema uchunguzi umabaini kuchanika kwenye maungio ya goti, lakini jeraha hilo halifanani na lile lililomuweka nje miezi saba kwenye msimu huu.