
Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Bayern Munich, David Alaba.
Alaba ameyasema hayo mchana wa leo Mei 6, 2021 wakati alipokuwa anafanya mahojiano maalumu na gazeti la klabu hiyo “Magazine 51” juu ya uamuzi wake wa kuondoka klabu hapo nakuelezwa kutimkia miamba ya soka ya nchini Hispania, klabu ya Real Madrid.
Alaba amesema,“Ili uweze kukua, unapaswa kutoka kwenye mazingira uliyoyazoe. Nafikiri hivyo, utoke uende mahali ambapo hujulikani ili ukomae tena”.Bado kuna muda kabla sijaondoka, na siwezi kujizuia, kwa kipindi chote ilikuwa miaka mizuri sana”.
“Nitaondoka Bayern na machozi machoni mwangu lakini, nafikiria muda huo huo nafikiria maisha yangu ya baadae. Ninajivunia kwakiasi kikubwa sana. Ninawatakia Bayern iendelee kuandika historia kubwa za mafanikio”.
Alaba ataondoka Bayern kuelekea Madrid akiwa ni miongoni mwa mashujaa wa klabu hiyo akitoa mchango mkubwa sana kwenye mafanikio ya klabu hiyo ikiwemo kubeba mataji matatu makubwa ‘Treble’ mara mbili, mwaka 2013 na msimu wa mwaka 2019-2020.