Jumamosi , 25th Mei , 2019

Msemaji wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, siku za hivi karibuni amekuwa akitoa elimu ya uwekezaji kwa vilavu kongwe vya Yanga na Simba huku akikosoa baadhi ya mambo.

Leo amekosoa timu hizo kuitwa timu kubwa ilihali hazina uhalisia wa kuwa hivyo kutokana na namna ambavyo vinajiendesha.

''Hivi kweli Simba na Yanga ni timu kubwa? Hatuna viwanja vya mechi wala mazoezi, hatuna academy, hatuna Malls. Mafanikio makubwa iliyonayo FC Barcelona ni matokeo ya uwepo wa kituo cha kukuzia vipaji cha La Masia'', amesema.

Aidha Dismas amezipa changamoto klabu hizo kwa kusema kujiuliza ni watoto wangapi nchini wangependa kupita kwenye 'academy' za Simba na Yanga, ni vipaji vingapi vingevumbuliwa nchini kupitia Simba na Yanga. Wachezaji vijana wangapi wangeuzwa ndani na nje ya nchi kutoka kwenye 'academy' za Simba na Yanga.

Simba na Yanga ni timu zilizoanzishwa miaka ya 1930 lakini mpaka sasa havijafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa barani Afrika ambapo mbali na Simba kufika fainali ya kombe la shirikisho miaka ya nyuma hakuna timu imeweza kuchukua kombe.